Jumamosi, 16 Januari 2016

KUHUSU GREAT COMMISSION AFRICA

Great  Commision Africa ni shirika la kidini lenye malengo kusaidia jamii nchini Tanzania, Africa, na Ulimwangu kote. Hili ni agizo kuu la Bwana Yesu Kristo, Yesu anasema katika injili ya Mathayo Biblia inasema "Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, ........... 28:19- 20

Maono ya Great Commission Africa (GCA) nikuufikia Ulimwengu kwa kila upande, kufika kusiko fikika (Reaching unreachable)  Tunafahamu ni kwa namna gani ulimwengu unahitaji msaada  kwa kila namna, kuna jamii iliyoko vijijini na zaidi ya vijijini yani Polini ( Bush) wanahitaji msaada wa kiafya, kielimu, pamoja na  misaada mingine ya kiutu.

Kwa miaka mitano sasa  Great Commission Africa (GCA) imewafikia watu wengi katika kupeleka neno la Mungu na misaada  mingine ya kiutu  katika maeneo mbalimbali mjini na vijijini.

Biblia inseama katika kitabu cha Yakobo. " Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwande kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, ....... Yakobo 1:27"

Kila mtu ano wajibu wa kumsaidia mtu mhitaji kwa namna yoyote. Hebu fikiria ni kwa namna gani Mungu amekubariki. amekupatia vitu vingi zaidi ya ndugu nyako au  jirani yako. Kila mmoja kwa namna ya tofauti tofauti tumepewa baraka nyingi sana na Mungu. yaweza kuwa baraka za Mali au marifa (Ujuzi), karama za Mungu (Roho Mtakatifu) namna mbalimbali. tunahitaji kuwa waminifu katika kuwasaidia watu wengine katika maeneo tofautitofauti. Bila kujali rangi, kabila, jinsia, au taifa.

Sisi sote tumeubwa kwa mfano wa Mungu ndivyo maandiko ya mwenyezi Mungu yana sema katika kitabu cha Mwanzo " Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu,....... Mwanzo 1: 26. Lazima dhamira ya kila mmoja iwe ni kuwa na moyo wa huruma, moyowa kuwahurumia wengine, huruma yetu huzihilika kaika matendo siyo maneno tu. " Vivyo hivyo na imani isipo kuwa na matendo imekufa........... Yakobo 2: 17"

Great Commission Africa tunayo dhamila ya dhati katika kusaidia jamii kiroho na kimwili pia. tunayo dhamira  ya kutoa elimu yenye lengo la kuleleta mabadiliko ndani ya jamii katika kujenga uelewa wa kina kuhusu mpango wa Mungu kuhusu mwanadamu namna tunavyo hitaji kuishi maisha ya kusaidiana kila mmoja, bila kujali kiwango cha uchumi.

Unaweza kushiriki kwa njia moja au nyingine katika kuleta mabadiliko ndani ya jamii. Tunaamini unacho kitu kwa ajili yakuwasidia watu wengine. ili kupata kujua namna unavyo weza kufanya tafadhali wasiliana nasi ili kukuelekeza namna unavyo weza kufanya.Pia unaweza kuungana na timu ya Great Commission Africa (GCA)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni