Obeid K. Mayinza (KK) The co-founder and the President of Great Commission Africa - Tanzania.
Alizaliwa mwaka 1978 mkoani Tabora, alipata maona ya umisheni tangu 1997 wakati huo alikuwa akiishi mkoa wa Tabora, amefanya huduma ya uinjilisti hasa katika maeneo ya vijijini katika mikoa mbalimbali ya nchini Tanzania. Kufikia mwaka 2015 amefikia vijiji zaidi ya 550 katika maeneo tofauti tofauti nchini Tanzania pamoja na nchi za jirani ya Tanzania, Kenya, Burundi, Uganda, Rwanda na DRC Congo.
Msukumo wake ni kufika kusiko fikika. (Reaching unreachable) Mwanzilishi huyu aligundua kuwa Ulimwengu unahitaji dhamira ya dhati katika kufikia maeneo tofauti tofauti. kile ambacho mwazilishi amekuwa akifanya ni kupeleka timu ya wainjilisti katika maeneo mbalimbali, mijini na vijijini. Ukweli ni kwamba kuna mambo mkubwa ambayo yametokea katika maeneo mbalimbali hapa Africa kupitia huduma ya Great Commission Africa.
Obeid K Mayinza(KK) kupitia huduma hii ana amini kuwa njia pekee ya kuufikia ulimwengu ni lazima Kanisa lipate nguvu na msukumo wa kuwafundisha wakristo kwa habari ya Umisheni.
Kwa hali ya kawaida kazi ya Umisheni ni kazi ambayo siyo ya rahisi sana, kwa kuwa inakufanya kuondoka mahali ambapo umepazoea na kwenda mahali pengine, na kukutana na watu tofauti ya wale uliowazoea na kukutana na changamoto nyingi, lakini jambo la mhimu ni lazima kukukumbuka kwamba tumeagizwa na Yesu Kristo (Mathayo 28:19- 20) hinyo jambo hili ni jambo la lazima sana kwa sababu ni agizo kuu.
Ikiwa kanisa litachukuwa hatua ya dhati kabisa katika kuelekeza nguvu katika Umisheni, yanaweza kutokea mabadiliko mkubwa sana katika ulumwengu. kwa sabu wokovu ni ufunguo mkuu wa ufahamu kwa mwanadamu
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni